SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: BOCCO AFURAHIA SAPOTI WANAYOPATA KUTOKA KWA MASHABIKI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nahodha wa timu ya Simba amekiri kufurahi baada ya mashabiki wengi kujitokeza katika michezo yao ya mbalimbali kunawapa motisha kufanya v...
Nahodha wa timu ya Simba amekiri kufurahi baada ya mashabiki wengi kujitokeza katika michezo yao ya mbalimbali kunawapa motisha kufanya vizuri uwanjani.

Bocco alitoa kauli hiyo baada ya kukabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari na kundi la Simba Sporaa baada ya kumalizika kwa mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Boko Veteran jioni ya leo.

Bocco amekabidhiwa pesa taslimu sh laki tano na fremu yenye picha yake kama sehemu ya zawadi hiyo.

Nahodha huyo alikuwa akabidhiwe zawadi hiyo jana baada ya mchezo huo dhidi ya Mtibwa Sugar lakini ilishindikana kufuatia idadi kubwa ya mashabiki kuingia uwanjani  huku mvua ikinyesha.

"Kwakweli mashabiki wetu wanatupa sapoti kubwa tunawashukuru sana na ninawaomba waendelee kufanya hivyo mpaka mwisho wa msimu.

"Hata zawadi hizi mnazotupata zinaendelea kutupa motisha kujituma uwanjani ili kuisaidia Simba kufanya vizuri na nawaomba msiishie hapa," alisema Bocco.

Mshambuliji huyo tayari amefunga mabao 12 kwenye ligi mpaka sasa akizidiwa matano na Emmanuel Okwi ambaye ndio kinara wa ufungaji.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top