Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi jioni hii katika uwanja wa Boko Veteran kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City utakaofanyika uwanja wa Taifa siku ya Alhamisi.
Wekundu hao walirejea usiku wa jana kutoka mkoani Morogoro baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri.
Katika mazoezi hayo yaliyosimamiwa na kocha Pierre Lechantre karibia wachezaji wote waliosajiliwa msimu huu walihudhuria isipokuwa Aishi Manula aliyefiwa na dada yake Juuko Murshid ambaye mke wake amejifungua.
Katika mchezo wa jana Simba ilikosa huduma ya Erasto Nyoni, James Kotei na Juuko Murshid kutokana na kuwa na kadi tatu za njano lakini tayari wamerejea kwa ajili ya mchezo dhidi ya City.
BAADA YA MTIBWA, SIMBA YAANZA MAWINDO YA MBEYA CITY
Title: BAADA YA MTIBWA, SIMBA YAANZA MAWINDO YA MBEYA CITY
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi jioni hii katika uwanja wa Boko Veteran kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City utakaofanyi...
Post a Comment