Liverpool imetiupa nje ya Manchester City katika michuano ya ligi mabingwa Ulaya baada ya kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika uwanja wa Etihad.
Majogoo hao wamewatoa City kwa jumla ya mabao 5-1 kufuatia kupata ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja Anfield Jumatano iliyopita.
City walipata bao la mapema dakika ya pili lililofungwa na Gabriel Jesus baada ya kupokea pasi ya Rahim Sterling lililodumu hadi mapumziko.
Mohammed Salah aliisawazishia Liverpool bao hilo dakika ya 56 kabla ya Roberto Firmino kuongeza la pili dakika ya 77.
Mchezo mwingine Barcelona imetupwa nje ya michuano hiyo na AS Roma baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Nou Camp, Barca iliishinda mabao 4-1 hivyo wametolewa kwa faida ya bao la ugenini.
Mabao ya Roma yalifungwa na Edin Dzeko dakika ya sita, Daniel De Rossi (58) na Kelvin Minolas (82).
Kesho kutakuwa na mechi mbili kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus wakati Bayern Munich itacheza na Sevilla.
LIVERPOOL YAIPIGA MAN CITY NJE NDANI, BARCA NAYO OUT ULAYA
Title: LIVERPOOL YAIPIGA MAN CITY NJE NDANI, BARCA NAYO OUT ULAYA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Liverpool imetiupa nje ya Manchester City katika michuano ya ligi mabingwa Ulaya baada ya kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali...
Post a Comment