Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga itakutana usiku wa leo kujadili suala kutimka kwa kocha wao George Lwandamina na kujiunga na Zesco United ya Zambia.
Taarifa zilizotolewa jana na klabu ya Zesco ni kwamba wamemalizana na kocha huyo ambaye anachukua mikoba ya kocha wa muda Tenant Chembo aliyejiuzulu siku ya Jumapili.
Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, Samwel Lukumai amesema baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi baina ya Yanga dhidi Singida United utakaofanyika uwanja wa Taifa jioni ya leo.
Lukumai ameongeza kuwa watahakikisha wanalipatia ufumbuzi mapema suala hilo ili lisiharibu mustakabali wao wa kutaka kutetea taji la ubingwa msimu huu.
"Siwezi kulizungumzia suala la Lwandamina kwa sasa kwakua leo kamati ya utendaji itakutana kujadili ili kulipatia ufumbuzi," alisema Lukumai.
YANGA KUKUTANA LEO KUJADILI SAKATA LA LWANDAMINA
Title: YANGA KUKUTANA LEO KUJADILI SAKATA LA LWANDAMINA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga itakutana usiku wa leo kujadili suala kutimka kwa kocha wao George Lwandamina na kujiunga na Zesco Un...
Post a Comment