SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SPORAA WAMCHAGUA BOCCO MCHEZAJI BORA FEBRUARI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kundi la Simba Sporaa limemtangaza nahodha wa timu hiyo John Bocco 'Adebayor' kuwa mchezaji bora kwa mwezi Februari. Huu ni utar...
Kundi la Simba Sporaa limemtangaza nahodha wa timu hiyo John Bocco 'Adebayor' kuwa mchezaji bora kwa mwezi Februari.

Huu ni utaratibu wa Sporaa kuchagua mchezaji bora wa Simba kila mwezi kwa ajili ya kuongeza motisha ndani ya timu na kuwafanya wachezaji kujituma zaidi.

Bocco ametengeneza uelewano mkubwa na Emmanuel Okwi ndani ya kikosi cha Simba na kuunda safu kali ya ushambuliaji ambayo inaongoza kwa kufunga mabao kwenye ligi.

Bocco atakabidhiwa pesa taslimu shilingi laki tano pamoja na fremu maalum yenye picha yake kama sehemu ya zawadi.

Nahodha huyo atakabidhiwa zawadi hiyo kesho kabla ya kuanza kwa mchezo wa ligi kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Simba utakaofanyika uwanja wa Jamhuri, Morogoro saa 10 jioni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top