Uongozi wa klabu ya Simba umekiri kuwa mchezo wa leo ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mgumu na wa kupendeza kutokana na ubora wa Wakata miwa hao.
Mchezo huo utakaofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo Mtibwa itaingia na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 iliyopata dhidi ya Singida United huku Simba ikiifunga Njombe Mji mabao 2-0.
Simba inahitaji pointi hizo kwa udi na uvumba ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa taji la ligi msimu huu baada ya kuukosa kwa miaka minne mfululizo.
Msemaji wa Simba, Hajji Manara amesema Mtibwa ni timu imara na wanatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mtibwa ingawa wao ni bora zaidi na wana uwezo kuondoka na pointi zote tatu.
Mara zote mechi ya Simba dhidi ya Mtibwa inakuwa ngumu kutokana na uchezaji wa timu hizo huku kipindi hiki wakiwa kwenye ubora mkubwa.
"Mechi itakuwa ngumu, Mtibwa ni timu bora na ina historia nzuri kwenye ligi, Simba tupo vizuri na tumejiandaa kuibuka na ushindi.
"Wachezaji wana morali ya hali ya juu na cha kushukuru hatuna hata mchezaji yoyote ambaye ni majeruhi," alisema Manara.
SIMBA: LEO TUNAKUTANA NA TIMU BORA
Title: SIMBA: LEO TUNAKUTANA NA TIMU BORA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa klabu ya Simba umekiri kuwa mchezo wa leo ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mgumu na wa kupendeza kutokana na ubora wa Wak...
Post a Comment