Kocha msaidizi wa timu ya Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema kuondoka kwa kocha mkuu George Lwandamina kumechangia kupata sare kwenye mchezo wa leo dhidi ya Singida United.
Nsajigwa amesema kuondoka kwa kocha huyo kumepunguza morali kwa wachezaji hali iliyopelekea kupata sare hiyo.
Sare ya leo imeifanya Yanga kuwa nyuma kwa pointi tano dhidi ya vinara Simba ambao kesho watacheza Mbeya City katika uwanja wa Taifa.
"Unajua hata kwenye familia anapo ondoka mtu ghafla tena baba lazima kutatokea tafauti lakini tutajipanga kukabiliana na hali hii nadhani hata kwenye sare hii imechangia.
"Binafsi sijapata taarifa rasmi kutoka kwa uongozi na suala hili lipo kwao nadhani watalipatia ufumbuzi haraka," alisema Nsajigwa.
Jana klabu ya Zesco ya Zambia ilimtangaza Lwandamina kuwa kocha wake mkuu baada ya kumalizana nae na atatangazwa rasmi siku chache zijazo.
NSAJIGWA AMTAJA LWANDAMINA SARE YA SINGIDA
Title: NSAJIGWA AMTAJA LWANDAMINA SARE YA SINGIDA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha msaidizi wa timu ya Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema kuondoka kwa kocha mkuu George Lwandamina kumechangia kupata sare kwenye mchezo...
Post a Comment