SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SINGIDA YAZIDI KUITIBULIA YANGA KATIKA MBIO ZA UBINGWA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Singida United imeibana mbavu Yanga baada ya kuilazimisha sare ya bao moja katika mchezo wa ligi uliofanyika uwanja wa Taifa na kujiweka k...
Singida United imeibana mbavu Yanga baada ya kuilazimisha sare ya bao moja katika mchezo wa ligi uliofanyika uwanja wa Taifa na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kutetea taji.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi 47 na kuendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa alama tano nyuma ya vinara Simba.

Singida walipata bao la mapema dakika ya pili lililofungwa na Salita Kambale baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kigi Makasi.

Mlinda mlango Ally Mustaph 'Barthez' na mlinzi Shafiq Batambuze walishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 40 baada ya kupata maumivu.

Baada ya kosa kosa nyingi langoni mwa  Singida hatimaye Yanga ilisawazisha bao hilo dakika ya 45 kupitia kwa mlinzi Abdallah Shaibu 'Ninja' kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ajib.

Kipindi cha pili Yanga waliongeza kasi na kuliandama lango la Singida lakini ubunifu ulikosekana kutoka safu ya kiungo kwenda kwa washambuliaji.

Singida iliwatoa Batambuze, Barthez na Nizar Khalifan nafasi zao zikachukuliwa na Salum Chuku, Manyika Junior na Yusuph Kagoma.

Kwa upande wa Yanga iliwapumzisha  Ajib na Pius Buswita na kuwaingiza Juma Mahadhi na Geofrey Mwashiuya.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top