Kocha mkuu wa timu ya Simba, Mfaransa Pierre Lechantre amevutiwa na mfumo wa kucheza soka la pasi fupi fupi unaochezwa na Singida United.
Lechantre alishuhudia mchezo kati ya Yanga na Singida jana katika uwanja wa Taifa uliomalizika kwa sare ya bao moja na kusema anapenda soka la kucheza soka la kuvutia.
Mfaransa huyo alisema alikwenda kushuhudia mechi hiyo kwakua ana mchezo dhidi yao na amechukua baadhi ya taarifa kutoka timu zote ambazo zitamsaidia watakapo kutana.
"Nimevutiwa na soka la Singida, wanacheza vizuri pasi fupi kwa nafasi lakini wana mapungufu ambayo nimeyaandika humu kwenye kitabu changu tutayafanyia kazi tukikutana.
"Yanga walicheza vizuri lakini walipoteza pasi na nafasi nyingi, sijajua kwanini ila nasikia imewakosa baadhi ya nyota wao muhimu," alisema Lechantre.
MFARANSA WA SIMBA AVUTIWA NA SOKA LA SINGIDA UNITED
Title: MFARANSA WA SIMBA AVUTIWA NA SOKA LA SINGIDA UNITED
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha mkuu wa timu ya Simba, Mfaransa Pierre Lechantre amevutiwa na mfumo wa kucheza soka la pasi fupi fupi unaochezwa na Singida United. ...
Post a Comment