Mtibwa Sugar imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 mbele ya Singida United katika mchezo wa ligi uliofanyika kwenye uwanja Namfua ambao haukutarajiwa na wadau wengi.
Mtibwa walikuwa kwenye kiwango bora wakimiliki sehemu kubwa ya mchezo huku Singida wakionekana kushindwa kuhimili vishindo vya Wakata miwa hao.
Ushindi huo ni kama salamu kwa Simba ambao watakutana siku ya Jumatatu Aprili 9 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Mshambuliji Kelvin Sabato 'Kiduku' aliifungia Mtibwa bao la kwanza dakika ya 22 kwa mpira wa adhabu uliomshinda mlinda mlango Ally Mustaph 'Barthez'.
Winga wa Salim Kihimbwa aliifungia Mtibwa bao la pili dakika ya 53 kabla ya Hassan Dilunga kufunga la mwisho dakika ya 71 kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi Ismail Aidan kuangushwa ndani ya 18.
Mchezo mwingine wa ligi uliofanyika leo Mbao FC imebanwa mbavu na Lipuli kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana.
MTIBWA YAIDUWAZA SINGIDA NAMFUA, YATUMA SALAMU SIMBA
Title: MTIBWA YAIDUWAZA SINGIDA NAMFUA, YATUMA SALAMU SIMBA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mtibwa Sugar imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 mbele ya Singida United katika mchezo wa ligi uliofanyika kwenye uwanja Namfua ambao hauku...
Post a Comment