SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: NAHODHA WA DICHA: NILIIFAHAMU YANGA KUPITIA BOSSOU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nahodha wa timu ya Wolaita Dicha, Djacko Arafat amesema alipata taarifa za Yanga kupitia kwa mlinzi wa zamani wa mabingwa hao Vincent Boss...
Nahodha wa timu ya Wolaita Dicha, Djacko Arafat amesema alipata taarifa za Yanga kupitia kwa mlinzi wa zamani wa mabingwa hao Vincent Bossou.

Djacko raia wa Togo amesema Bossou ambaye nae anatokea huko hajamwambia mambo mengi  kuhusu Yanga lakini hata hicho kidogo anachofahamu amewashirikisha wenzake ili kuisaidia timu kupata matokeo chanya.

Nahodha huyo ndio mchezaji pekee anayetoka nje ya Ethiopia akiwa amefunga mabao matano kwenye ligi na mawili kwenye kombe la Shirikisho Afrika.

"Bossou aliniambia mambo machache kuhusu Yanga, tunatarajia kupata upinzani mkubwa lakini tutahakikisha tunamaliza kazi huku ili nyumbani iwe rahisi kwetu," alisema Djacko.

Djacko aliongeza kuwa hali ya hewa ya Dar es Salaam ni joto sana tofauti na kwao lakini haitawaathiri kuelekea mchezo wa leo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top