Wakili wa Michael Wambura, Emmanuel Muga amesema walifahamu kuwa wasingeweza kushinda rufaa yao baada ya kubalishwa wajumbe wa Kamati ya Rufaa ya Maadili.
Wakili Muga amesema kubadilishwa wajumbe wa Kamati hiyo muda mfupi baada ya kukata rufaa ilionyesha isingekuwa rahisi kwa wao kupata haki yao.
Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF chini ya Mwenyekiti Ebenezer Mshana kutupilia mbali rufaa ya Wambura ya kutojihusisha na soka maisha.
Muga ameongeza kuwa mteja wake ataendelea kutafuta haki yake kwa njia ya yoyote na suala hilo bado halijamalizika ingawa hajaweka wazi njia watakazo tumia.
"Kwanza hatukuwa na imani na Kamati baada ya kubadili wajumbe, tulitegemea kabisa jambo hili kutokea lakini niwaambie jambo moja kuwa suala hili bado halikwisha," alisema Wakili Muga.
Wambura alihukumiwa Machi 15 na Kamati ya Maadili akituhumiwa makosa matatu likiwemo la kufanya vitendo vya kulichafua Shirikisho hilo.
MUGA: TULIJUA RUFAA YETU ITATUPILIWA MBALI
Title: MUGA: TULIJUA RUFAA YETU ITATUPILIWA MBALI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Wakili wa Michael Wambura, Emmanuel Muga amesema walifahamu kuwa wasingeweza kushinda rufaa yao baada ya kubalishwa wajumbe wa Kamati ya R...
Post a Comment