Kocha msaidizi wa timu ya Lipuli FC, Suleiman Matola
amesema wana tegemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa wenyeji wa Mbao FC
katika mchezo wa ligi kuu hii leo lakini wao ndio wataibuka na ushindi.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya Simba amesema Mbao
wapo kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi na wanafahamu watapambana kufa
na kupona kupata alama tatu lakini leo itakuwa ngumu kwao.
Mchezo huo utafanyika saa 10 jioni katika uwanja wa
CCM Kirumba ambao unatarajiwa kuwa wavute nikuvute kwa timu zote.
Mbao wamekuwa wakicheza vizuri sana wanapokuwa
katika uwanja huo na kuwapa shida wapinzani wao kitu ambacho Lipuli wanatarajia
kitatokea.
"Mbao wapo nafasi ya pili kutoka chini,
tunafahamu watataka kupata ushindi wa nyumbani ili kujinasua ingawa leo
tutawafunga," alisema Matola kwa kujiamini.
Lipuli ipo nafasi ya saba kwenye msimamo ikiwa na
pointi 27 wakati Mbao ikiwa nafasi ya 14 na alama zake 19.
Post a Comment