Kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps klabu ya Manchester United haipo tayari kumuuza winga wake Anthony Martial kwenda Juventus mwishoni mwa msimu huu.
Martial amekuwa akiingia na kutoka kwenye kikosi cha kocha Jose Mourinho at Old Trafford na ameanza mechi 16 pekee msimu huu.
Iliripotiwa kuwa United ipo tayari kumruhusu winga huyo baada kutaka saini ya nyota wa Real Madrid, Gareth Bale kitu ambacho kinawafanya Juve kujiandaa kupeleka ofa.
Deschamps amesema anaamini Juve watapeleka ofa kubwa kwa United ingawa haoni kama Mashetani hao watakubali kumuachia nyota huyo wa zamani wa Monaco.
"Martial ana mkataba na United na klabu haipo tayari kumuuza, tutaona huko mbeleni.
"Mimi sikumpa ushauri ila nimempa maoni mwisho wa siku mwamuzi wa mwisho ni mchezaji mwenyewe," alisema Deschamps.
Martial ameshinda taji FA, EFL na Europa tangu ajiunge na United kwa dau la pauni 58 milioni.
DESCHAMPS ASEMA UNITED HAITA MUUZA MARTIAL, JUVENTUS
Title: DESCHAMPS ASEMA UNITED HAITA MUUZA MARTIAL, JUVENTUS
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps klabu ya Manchester United haipo tayari kumuuza winga wake Anthony Mart...
Post a Comment