SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: TFF YATUPILIA MBALI RUFAA YA WAMBURA, KIFUNGO KIPO PALE PALE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kamati ya Maadili ya Rufaa ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imetupilia mbali Rufaa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho...
Kamati ya Maadili ya Rufaa ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imetupilia mbali Rufaa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Michael Wambura ya kufungiwa maisha kujihusisha na soka.

Akisoma hukumu hiyo ambayo ilichukua zaidi ya saa moja na nusu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Ebenezer Mshana amesema Mawakili wa mrufani walishindwa kujibu hoja za mteja wao badala yake wakajikita kuzungumzia utaratibu uliotumika.

Wambura alihukumiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, Machi 15 kwa makosa matatu ambayo ni kupokea pesa za malipo yasio halali kinyume na sheria, Kughushi barua ya kampuni ya JEKC ili kulipwa isivyo halali na kufanya vitendo vilivyovunja hadhi ya TFF.

Wakili Mshana amesema licha ya jopo la Mawakili wa Wambura kupewa muda mrefu wa kumtetea mteja wao lakini walishindwa kufanya hivyo na kamati yake imeridhia hukumu iliyotolewa na Kamati ya Maadili na kumtaka Wambura kuendelea na adhabu ya kufungiwa maisha.

"Baada ya kupitia vielelezo vyote vilivyoletwa mbele yetu kutoka kwa mrufani na TFF tumejiridhisha kuwa Wambura na jopo lake la Mawakili walishindwa kujibu hoja za msingi na kujitikita katika utaratibu uliotumika.

"Katika zile hoja tatu alizotuhumiwa nazo hakuna sehemu yoyote kwenye ushaidi wao ambayo walikanusha kutenda kosa hilo, hivyo kamati yangu imeridhia bila shaka na hukumu iliyotolewa awali na Kamati ya nidhamu," alisema Wakili Mshana.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top