SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: YANGA YAAHIDI KUIMALIZA DICHA NYUMBANI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Yanga inajipanga kuhakikisha inashinda mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha ya Ethiopia ili kujiw...
Timu ya Yanga inajipanga kuhakikisha inashinda mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha ya Ethiopia ili kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye mechi ya marudiano.

Mabingwa hao wamekuwa wakishindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani kwenye michuano ya kimataifa na kujitahidi kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano.

Yanga ilitolewa kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika na Township Rollers ya Botswana kwa jumla ya mabao 2-1 yaliyopatikana kwenye uwanja wa Taifa kabla ya kutoka sare ya bila kufungana jijini Gaborone.

Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, Samwel Lukumai amesema safari hii hawatakubali kurudia makosa watahakikisha wanashinda nyumbani.

"Kikubwa tumewafahamu wapinzani wetu na mechi ya kwanza tutaanzia hapa nyumbani na leo tutakuwa na kikao kujadili mechi hiyo, kikubwa ni kuhakikisha tunashinda hapa nyumbani," alisema Lukumai.

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo utafanyika Aprili 6-8 jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana Aprili 16-17 nchini Ethiopia.

Hata kikosi cha mabingwa hao kitaingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya Singida United, Aprili mosi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top