SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: NINJE ARIDHISHWA NA VIWANGO VYA VIJANA WAKE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Ammy Ninje ameridhishwa na viwango vilivyo onyeshwa na vijana hao ...
Kocha wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Ammy Ninje ameridhishwa na viwango vilivyo onyeshwa na vijana hao kwa muda mfupi waliokaa nao.

Ninje alipewa kibarua hicho Jumanne ya wiki iliyopita na kuingoza kupata ushindi kwenye mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya Morocco na Msumbiji.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuinoa timu ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Chalenji iliyofanyika nchini Kenya mwaka jana amesema angependa kupata mechi nyingine ya kirafiki kama itawezekana.

"Vijana wameonyesha kiwango bora sana na ningependa nipate mechi nyingine ya kirafiki kabla ya kucheza mechi ya kufuzu lakini sina uhakika kama itapatikana," alisema Ninge.

Ngorongoro itacheza na DR Congo Machi 30 katika mchezo wa kufuzu mataifa Afrika kwa vijana utaofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top