Kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 'Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje ameendelea kuwapa raha Watanzania baada ya kukiongoza kikosi hicho kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Msumbiji.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa umefanyika kwenye uwanja wa Taifa ukiwa ni wapili mfululizo kwa Ninje tangu apewe kikosi hicho.
Ngorongoro ambayo inaundwa na wachezaji wengi waliokuwa Serengeti boys imeonyesha uwezo mkubwa kwenye mchezo huo kitu ambacho kinafanya Ninje kuhitaji kupewa muda zaidi kukijenga zaidi.
Msumbiji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 13 kupitia kwa Lionel Victor kabla ya Abdul Seleman kusawazisha dakika ya 35.
Winga Said Musa ambaye anachezea Yanga ndiye alifunga bao la ushindi dakika ya 71 akiihakikishia Ngorongoro kubaki na alama zote tatu.
Wiki iliyopita vijana hao walipata ushindi wa bao mbele ya Morocco katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
NINJE AZIDI KUWAPA RAHA WATANZANIA
Title: NINJE AZIDI KUWAPA RAHA WATANZANIA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 'Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje ameendelea kuwapa raha Watanzania baada ya kukiongoza...
Post a Comment