Gwiji wa Arsenal, Ian Wright anaamini Liverpool ikimpoteza Mohammed Salah wataumia sana kuliko ilivyokuwa kwa Phillipe Coutinho baada ya raia huyo wa Misri kutakiwa na Real Madrid.
Salah amekuwa kwenye kiwango bora tangu ajiunge na Liverpool akitokea Roma na tayari amefunga mabao 36 kwenye michuano yote msimu huu.
Madrid wamekuwa wakivutiwa na Salah ambapo mabao manne aliyofunga kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Watford siku ya Jumamosi yamezidi kuongeza tetesi huku Barcelona wakihitaji saini yake.
"Salah ni mchezaji mzuri na muhimu kwa Liverpool kwa sasa ikitokea akaondoka Majogoo hao wataumia sana kuliko ilivyokuwa kwa Coutinho.
"Sio kama siiheshimu Liverpool ila kama kweli Madrid watapeleka ofa sidhani kama Salah atakataa na kumpoteza nyota huyu itawauma sana kuliko Coutinho," alisema Wright.
Hata hivyo Liverpool wenyewe hawako tayari kumuuza nyota huyo kwa dau lolote.
WRIGHT: LIVERPOOL ITAUMIA KUMPOTEZA SALAH KULIKO COUTINHO
Title: WRIGHT: LIVERPOOL ITAUMIA KUMPOTEZA SALAH KULIKO COUTINHO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Gwiji wa Arsenal, Ian Wright anaamini Liverpool ikimpoteza Mohammed Salah wataumia sana kuliko ilivyokuwa kwa Phillipe Coutinho baada ya r...
Post a Comment