SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: YANGA HIYOO ROBO FAINALI ASFC
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Yanga imekuwa ya tano kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation...
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Yanga imekuwa ya tano kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuifunga Majimaji mabao 2-1.

Matokeo hayo yalitegemewa na wadau wengi wa soka kutokana na Majimaji kukumbwa na mgogoro wa ndani uliopelekea baadhi ya wachezaji kusimamishwa.

Licha ya sakata hilo Majimaji waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na nia ya kutafuta ushindi lakini sehemu ya umaliziaji ilikosa ubunifu.

Yanga ilienda mapumziko ikiwa mbele kwa bao moja lililofungwa na Pius Buswita kwa kichwa baada ya kupokea pasi ndefu ya Hajji Mwinyi dakika ya 40.

Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 57 lililofungwa na Emmanuel Martin akimalizia krosi ya Hassan Kessi.

Majimaji walipata bao la kufuatia machozi dakika ya 61 lililofungwa na Jafar Mohammed kwa kichwa baada ya kupokea mpira wa adhabu uliopigwa na Aziz Sibo.

Timu nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni Njombe Mji, Singida United, Mtibwa Sugar na Azam FC.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top