Mshambuliaji Romelu Lukaku ameiwezesha Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Chelsea katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliofanyika kwenye uwanja wa Old Trafford.
Ushindi huo umeifanya United kurejea nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 59 na kuishusha Liverpool iliyokuwa imekalia nafasi hiyo kwa muda kufuatia kuifunga West Ham United mabao 4-1 jana.
Lukaku aliifungia United bao la kusawazisha dakika ya 39 kufuatia kupokea pasi kutoka kwa Anthony Martial ndani ya 18.
Raia huyo wa Ubelgiji ambaye alikuwa kwenye kiwango bora siku ya leo alitengeneza bao la ushindi lililofungwa na Jesse Lingard dakika ya 74, nyota huyo alipiga mashuti mawili makali ambayo yaliokolewa na mlinda mlango Thibaut Courtious.
Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Willian dakika ya 31 baada ya kupokea pasi ya Eden Hazard na kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango David De Gea.
LUKAKU ANG'ARA UNITED IKIICHAPA CHELSEA OLD TRAFFORD
Title: LUKAKU ANG'ARA UNITED IKIICHAPA CHELSEA OLD TRAFFORD
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji Romelu Lukaku ameiwezesha Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Chelsea katika mchezo wa ligi kuu nchini...
Post a Comment