SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: GUARDIOLA AANZA KUFUNGUA KABATI ETIHAD
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amepata taji lake la kwanza akiwa na matajiri hao baada ya kuifunga Arsenal mabao 3-0 kwenye mche...
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amepata taji lake la kwanza akiwa na matajiri hao baada ya kuifunga Arsenal mabao 3-0 kwenye mchezo wa fainali wa Carabao.

Meneja huyo alitwaa jumla mataji 21 ikiwa na timu za Barcelona na Bayern Munich huku msimu wake wa kwanza nchini Uingereza akiambulia patupu.

City ndio vinara wa ligi kuu nchini humo ikiwa na alama 72 na inapewa nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa kutokana na kuwa na pointi 13 mbele huku ikiwa na mechi moja mkononi.

Mabao ya Man City yalifungwa na Sergio Aguero, Vincent Kompany na David Silva.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top