Timu ya Mbao FC imejidhatiti kuhakikisha inaisimamisha Simba kwa kuifunga kwenye mchezo wa ligi kuu utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa, jioni ya leo.
Simba ambayo ndio vinara wa ligi hiyo wamekuwa bora zaidi wanapocheza katika uwanja huo kutokana na sehemu yake ya kuchezea kuwa nzuri ikiwaruhusu kucheza pasi fupi fupi zinazo wasumbua wapinzani.
Mwenyekiti wa klabu ya Mbao, Solly Zephaniah amesema mchezo huo utakuwa wa kawaida na maandalizi yake yamekamilika na wana matumaini ya kuondoka na pointi zote tatu.
"Mchezo tunauchulia kawaida kama mechi nyingine, tumejiandaa vizuri na dhamira yetu ni kutoka na ushindi na hilo lipo ndani ya uwezo wetu," alisema Mwenyekiti huyo kwa kujiamini.
Mbao imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika michezo dhidi ya miamba soka nchini timu za Simba na Yanga hasa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Kirumba timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 huku Mbao ikitokea nyuma na kusawazisha.
MBAO 'FULL CONFIDENCE' MBELE YA MNYAMA LEO TAIFA
Title: MBAO 'FULL CONFIDENCE' MBELE YA MNYAMA LEO TAIFA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Mbao FC imejidhatiti kuhakikisha inaisimamisha Simba kwa kuifunga kwenye mchezo wa ligi kuu utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa, ...
Post a Comment