SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MTIBWA YAIPIGA MKWARA YANGA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Ushindi wa mabao 3-0 iliyopata Mtibwa Sugar dhidi ya timu ya Buseresere FC kutoka mkoani Mara umewapa motisha wa kufanya vizuri katika mch...
Ushindi wa mabao 3-0 iliyopata Mtibwa Sugar dhidi ya timu ya Buseresere FC kutoka mkoani Mara umewapa motisha wa kufanya vizuri katika mchezo ujao wa ligi dhidi ya mabingwa watetezi Yanga.

Mtibwa itaikaribisha Yanga, Jumamosi ya Machi 3 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ikiamini itaibuka na ushindi.

Kabla ya mchezo wa jana Mtibwa ilikuwa imepokea vipigo vya mfululizo ikiwemo kile cha bao moja kutoka kwa Maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Manungu.

Msemaji wa Wakata miwa hao, Thobias Kifaru amejigamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo wakichagizwa na ushindi uliowafanya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya FA kama wapinzani wao Yanga.

"Baada ya ushindi wa Buseresere tunarejea nyumbani kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Yanga Jumamosi ijayo, tunaamini tutabaki na pointi zote tatu na Yanga hawataamini kitakacho tokea," alisema Kifaru.

Kifaru amesema timu hiyo ipo safarini muda huu kutoka mkoani Mwanza kurejea Morogoro baada ya kumaliza mechi ya jana iliyopigwa kwenye uwanja wa Nyamagana.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top