Mtibwa Sugar imekuwa timu ya nne kutinga robo fainali ya michuano ya kombe FA baada ya Njombe Mji, Singida United na Azam FC kufuatia kuifunga timu ya Buseresere kutoka Mara mabao 3-0 katika uwanja wa Nyamagana.
Mtibwa haikuwa na matokeo mazuri katika mechi zake za karibuni ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao moja kutoka kwa Maafande wa Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu.
Katika mchezo huo mabao ya Mtibwa yalifungwa na Hassan Dilunga kwa mkwaju wa penati, Haruna Chanongo na Ally Makarani.
Buseresere ndio timu pekee bingwa wa mkoa iliyokuwa imebaki katika michuano hiyo.
Muda mfupi ujao Majimaji itakutana na mabingwa watetezi wa ligi kuu timu ya Yanga katika muendelezo wa michuano hiyo.
MTIBWA YAZIFUATA AZAM, SINGIDA ROBO FAINALI FA
Title: MTIBWA YAZIFUATA AZAM, SINGIDA ROBO FAINALI FA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mtibwa Sugar imekuwa timu ya nne kutinga robo fainali ya michuano ya kombe FA baada ya Njombe Mji, Singida United na Azam FC kufuatia kuif...
Post a Comment