SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KMC MMEWASIKIA AZAM WANAVYOSEMA?
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Azam FC imesema itaingia katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) utakaofanyika leo jioni ikiwa na leng...

Azam FC imesema itaingia katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) utakaofanyika leo jioni ikiwa na lengo moja la kushinda ili kufuzu  hatua ya robo fainali.

Mchezo huo utaanza saa 1 jioni katika kwenye uwanja wa Azam Complex huku KMC ikiwa mwenyeji wa Wana lamba lamba hao 

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema wanafahamu kuwa mchezo huo utakuwa mgumu na wanawaheshimu wapinzani wao lakini kesho wajiandae kutolewa kwenye michuano hiyo.

Jaffer amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri isipokuwa wataendelea kukosa huduma ya nahodha wao Himid Mao ambaye amerejea kutoka Afrika Kusini kupata matibabu ya goti.

"Michuano ya FA siku zote haina sare wala marudiano lazima mmoja afungwe nasi tunalijua ndio maana tumejipanga kuhakikisha tunashinda na wachezaji wametuahidi hilo.

"Maandalizi yalianza toka Jumatatu kwahiyo benchi la ufundi chini ya Aristica Cioba linasema kila kitu kimeenda sawa na wachezaji wapo tayari kwa mchezo," alisema Jaffer.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top