Yanga imesonga mbele
katika hatua ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuitoa
St Louis ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 2-1 na imerejea nchini usiku wa jana
ikitokea visiwani humo.
Katibu mkuu wa klabu
hiyo, Boniface Mkwasa amesema wachezaji wamepumzika leo na kesho watasafiri
kuelekea Songea kwa ajili ya mchezo wa FA dhidi ya Majimaji siku ya Jumapili.
Mkwasa amesema baada
ya mchezo wa Majimaji timu itasafiri kwenda mkoani Mtwara kucheza mechi ya ligi
dhidi ya Ndanda kabla ya kwenda Morogoro kucheza na Mtibwa na kurejea jijini
Dar es Salaam kukutana na Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa kwanza
wa ligi ya mabingwa Afrika.
"Ratiba ni ngumu
wachezaji hawana muda wa kupumzika tunacheza mechi mfululizo, tutaiandikia
barua Bodi ya ligi ili kuangalia watatusaidiaje katika hili. Tunasafiri umbali
mrefu na miundo mbinu ya barabara zetu sio rafiki sana" alisema Mkwasa.
Licha ya ratiba hiyo
kubana Yanga pia inaandamwa na idadi kubwa ya majeruhi ya wachezaji wake nyota.
Post a Comment