Chelsea itawakosa
nyota wake David Luiz, Tiemoue Bakayoko na Ross Barkley katika mchezo wa kesho
wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Old
Trafford.
Luiz anaandamwa na
majeruhi ambapo amecheza mechi nne katika michezo 13 ya Chelsea mwaka huu
wakati Bakayoko akiwa nae akiumia mapema mwezi huu.
Barkley alicheza mara
ya mwisho mwezi iliyopita katika mchezo dhidi ya Arsenal uliomalizika kwa
kipigo cha mabao 2-1.
Meneja wa Chelsea
Antonio Conte amesema wachezaji hao wote hawatakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya
United, “Hapana hawatacheza, lakini hakuna mchezaji mwingine atakaye kosekana
baada ya hao wote wako vizuri.”
Chelsea imepoteza
michezo miwili mfululizo ya ligi mwezi uliopita ikiwa nafasi ya nne kwenye
msimamo huku ikiizidi pointi moja Tottenham Hotspur iliyo nafasi ya tano.
Post a Comment