SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: AZAM NAYO YATINGA ROBO FAINALI FA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Azam FC imekuwa timu ya tatu kutinga robo fainali ya michuano ya FA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC mchezo uliopigwa...
Azam FC imekuwa timu ya tatu kutinga robo fainali ya michuano ya FA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC mchezo uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex muda mfupi uliopita.

Njombe Mji ilikuwa ya kwanza kutinga hatua hiyo baada ya kuitoa Mbao FC ikafuatiwa na Singida United iliyoitoa Polisi Tanzania jioni ya leo.

Katika mchezo wa leo Azam ilitawala sehemu kubwa ya mchezo na ilifanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Frank Domayo dakika ya kwanza tu.

Mabao mengine ya Azam yalifungwa na washambuliaji Mbaraka Yusuph na Yahya Zayd huku lile la KMC likifungwa na Mohammed Hassan.

Mchezo huo ulitarajiwa kuwa mgumu zaidi Azam kutokana na kasi waliomalizia KMC katika ligi daraja la kwanza lakini ikawa rahisi kwa upande wao.

Timu tano zitaungana na Njombe, Azam na Singida katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo huku mechi nyingine zikipigwa kesho.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top