SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: WENGER AMTEGEMEA AUBAMEYANG KUIA CITY LEO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini mshambuliji wake mpya Pierre-Emerick Aubameyang atakuwa na kasi zaidi kwenye mchezo wa fainali w...
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini mshambuliji wake mpya Pierre-Emerick Aubameyang atakuwa na kasi zaidi kwenye mchezo wa fainali wa kombe la Carabao dhidi ya Manchester City.

Nyota huyo anayeshikilia rekodi ya kusajiliwa kwa dau kubwa alifunga bao lake la kwanza katika mchezo dhidi ya Everton na anategemewa kuwa mwiba kwa vijana wa Pep Guadiola.

Aubameyang hana vigezo vya kuitumikia Arsenal kwenye michuano ya Europa na hakucheza mechi yoyote tangu wapokee kichapo cha bao moja kutoka kwa Tottenham Hotspur huku Wenger akitajia raia huyo wa Gabon kuiumiza Man City leo kwenye uwanja wa Wembley.

"Amecheza mechi mbili tu, hakuwa fiti ndio maana alipewa mazoezi ya viungo ili kumjenga kwa wiki mbili sasa, nadhani leo atakuwa na kasi kuliko ilivyokuwa wiki kadhaa zilizopita," alisema Wenger.

Wakati Wenger akiamini Aubameyang atakuwa msaada mkubwa kwenye mchezo huo lakini itategemea na jinsi wachezaji wenzake watakavyokuwa kwakua wakati mwingine wanashindwa kuwa katika viwango bora.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top