SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: ZANZIBAR YAIFANYIA UNYAMA KILI STARS CHALENJI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Zanzibar Heroes imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya ndugu zao Kilimanjaro Stars na kukaa kileleni mwa kundi A kufuatia kushi...
Timu ya Zanzibar Heroes imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya ndugu zao Kilimanjaro Stars na kukaa kileleni mwa kundi A kufuatia kushinda michezo yote miwili ya kwanza.

Ushindi huo unaifanya Zanzibar kufikisha pointi sita wakati Kili Stars ipo mkiani mwa kundi ikiwa na alama moja na goli moja.

Zanzibar Heroes walianza mchezo huo kwa kasi kwa kushambulia zaidi lango la Kili wakitengeneza nafasi kadhaa ambazo ziliishia kwa walinzi au mlinda mlango Aishi Manula.

Nahodha Himid Mao aliipatia Kili bao la kwanza dakika ya 28 akimalizia pasi ya Danny Lyanga ambayo ndio ilikuwa nafasi ya kwanza kutengenezwa na vijana hao wa kocha Ammy Ninje.

Kassim Khamis aliyeingia muda mfupi kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya aliisawazishia Zanzibar dakika ya 66 baada ya beki Boniface Maganga kufanya uzembe.

Ibrahim Ahmada aliifungia Zanzibar bao la pili na ushindi dakika ya 78 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kassim Selembe.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top