SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MNYAMA KUJIPIMA KESHO NA KMC
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha timu ya Simba kitacheza mchezo wa kirafiki kesho dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) mchezo utakaofanyika kwenye uwan...
Kikosi cha timu ya Simba kitacheza mchezo wa kirafiki kesho dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex saa 1 usiku.

Simba nyota wake kadhaa wapo kwenye kikosi cha timu za Tanzania bara 'Kili Stars' kinachoshiriki michuano ya Cecafa Senior Challenge inayoendelea nchini Kenya.

Simba inatumia mechi hiyo kujiandaa na mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza pamoja na michuano ya Mapinduzi itakayoanza mapema mwezi ujao visiwani Zanzibar.

Nyota wa Simba waliopo kwenye kikosi cha Kili Stars ambao watakosa mchezo wa kesho ni Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein, Mzamiru Yassin, Jonas Mkude na Shiza Kichuya.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top