SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: RONALDO AMKUTA MESSI ATWAA BALLON D'OR YA TANO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nyota Cristiano amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mara ya tano na kumkuta mpinzani wake wa karibu Lionel Messi. Ronaldo raia ...
Nyota Cristiano amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mara ya tano na kumkuta mpinzani wake wa karibu Lionel Messi.

Ronaldo raia wa Ureno alikuwa na mwaka mzuri baada ya kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kutwaa ligi kuu ya Hispania, ligi ya mabingwa akiwa mfungaji bora msimu uliopita.

Ronaldo pia aliisaidia timu yake ya taifa ya Ureno kutwaa taji la Euro lililofanyika nchini Ufaransa mwezi Juni mwaka jana.

Kwa muongo mmoja Ronaldo na Messi wamekuwa wakipokezana tuzo hizo ambapo kwa sasa kila mmoja ametwaa tuzo hiyo mara tano.

Mara ya kwanza kwa Ronaldo kutwaa tuzo hiyo ilikuwa mwaka 2008 akiwa na klabu ya Manchester United.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top