Licha ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanzibar Heroes kocha wa Kilimanjaro Stars, Ammy Ninje amesema bado wana nafasi ya kusonga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Cecafa Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
Kipigo jana kimewakera wadau na mashabiki wa soka nchini ambao walikuwa na matarajio makubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ikiwezekana kutwaa taji hilo lakini matumaini yameanza kuyeyuka.
Kili Stars ina pointi moja ikibakiwa na michezo miwili wakati Zanzibar ikiwa na alama sita huku wenyeji Kenya wakiwa na pointi nne hali ambayo vijana wa Ninje wana kazi kubwa ya kufanya ili kufuzu hatua hiyo.
Kocha Ninje amesema kipindi cha kwanza walicheza vizuri na kufanikiwa kupata bao la kuongoza kabla ya wapinzani kubadilika na kusawazisha na kuongeza la pili huku wao wakipunguza kasi.
"Bado tuna nafasi ya kusonga mbele mechi zetu mbili zilizobaki tunaweza kushinda na kufuzu hatua ya nusu fainali. Nitawaweka wachezaji kwenye hali nzuri kisaikolojia ili kushinda michezo hiyo," alisema Ninje.
Kili Stars itashuka dimbani kesho kucheza na Rwanda 'Amavubi' ambayo imepoteza mechi mbili za awali dhidi ya Kenya na Zanzibar.
NINJE: BADO TUNA NAFASI YA KUSONGA MBELE CHALENJI
Title: NINJE: BADO TUNA NAFASI YA KUSONGA MBELE CHALENJI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Licha ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanzibar Heroes kocha wa Kilimanjaro Stars, Ammy Ninje amesema bado wana nafasi ya kusonga hatua ya n...
Post a Comment