SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: WENGER AITOA ARSENAL KWENYE MBIO ZA UBINGWA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa timu yake haina matumaini ya kutwaa taji la ligi msimu huu badala yake wameelekeza nguvu kwen...

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa timu yake haina matumaini ya kutwaa taji la ligi msimu huu badala yake wameelekeza nguvu kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Southampton.

Wenger amesema itakuwa sio uhalisia kwa Arsenal kufikiria ubingwa baada ya kipigo cha mabao 3-1 nyumbani dhidi ya  Manchester United wikiendi iliyopita.

Arsenal ipo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa nyuma kwa alama 15 mbele vinara Manchester City ambapo Wenger anatarajia kufanya mabadiliko kikosini katika mchezo wa St Mary mwishoni juma.

"Kwa sasa kuna vitu tunafikiria zaidi ya ubingwa, baada ya kipigo cha wikiendi tunaangalia kushinda mchezo ujao tu.

"Kuzungimzia ubingwa kwa sasa ni uongo, acha tujaribu kushinda mchezo wetu ujao ili tupunguze tofauti ya pointi labda baadae tunaweza kuwa vizuri zaidi," alisema Wenger.

Washika bunduki hao waliibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya BATE Borisov katika mchezo wa Europa uliofanyika kwenye uwanja wa Emirates jana.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top