Kiungo wa timu ya Singida United, Mudathir Yahaya amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba wa ligi kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.
Mudathir ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, beki Asante Kwasi wa Lipuli ya Iringa na mshambuliaji Danny Usengimana pia wa Singida alioingia nao fainali ya kuwania nafasi hiyo.
Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Singida mwezi huo ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Oktoba hadi ya nne.
Singida ilitoka 0-0 na Yanga, iliifunga Mbeya City mabao 2-1 na pia iliifunga Lipuli bao 1-0, ambapo Mudathir alicheza dakika zote 270 sawa na michezo mitatu na hakuwa na kadi yoyote.
Mudathir pia alitajwa mchezaji bora wa mchezo wa Singida United dhidi ya Yanga uliofanyika Uwanja wa Namfua uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.
Kiungo huyo kwa sasa yupo nchini Kenya ikiiwakilisha Zanzibar kwenye michuano ya Chalenji huku wakiwa vinara wa kundi A na pointi sita.
Mudathir atazawadiwa Sh milioni moja kutoka wadhamini Vodacom pamoja na kisimbusi (decoder) cha Azam kwa kuwa mchezaji bora wa mwezi.
MUDATHIR MCHEZAJI BORA VPL MWEZI NOVEMBA
Title: MUDATHIR MCHEZAJI BORA VPL MWEZI NOVEMBA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo wa timu ya Singida United, Mudathir Yahaya amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba wa ligi kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania B...
Post a Comment