SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MGHANA MPYA WA AZAM KUANZA KESHO NA FRIENDS RANGERS
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji mpya wa Azam FC raia wa Ghana Bernard Arthur ataonekana kwa mara ya kwanza na jezi ya Wana lamba lamba hao kesho katika mchez...
Mshambuliaji mpya wa Azam FC raia wa Ghana Bernard Arthur ataonekana kwa mara ya kwanza na jezi ya Wana lamba lamba hao kesho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers.

Mchezaji huyo alisajiliwa mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Mghana mwenzake Yahaya Mohammed aliyevunjiwa mkataba kutokana na kushindwa kufunga.

Arthur amefanya mazoezi na wachezaji wenzake kuanzia wiki iliyopita na kesho ataonekana kwa mara ya kwanza katika mchezo kama yuko vizuri au wa kawaida.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amewataka mashabiki wa timu kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwapa nguvu wachezaji ili kuibuka na ushindi.

"Kesho saa 1 usiku tutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends utakaofanyika kwenye uwanja wetu wa Azam Complex, nichukue nafasi hii kuwakaribisha wapenzi kujitokeza kwa wingi ili kuwapa nguvu katika mchezo huo.

"Mshambuliaji wetu mpya Bernard Arthur nae atakuwa mmoja wa nyota wataocheza mchezo huo kwahiyo itakuwa vizuri kwa mashabiki kumuona uwezo wake katika mchezo huo," alisema Jaffer.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top