Timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) imeanza kwa sare michuano ya Cecafa Senior Challenge baada ya kubanwa mbavu na Burundi (Intamba Murugamba) katika mchezo wa kundi B.
Mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Bukhungu katika mji wa Kakamega ulishuhudiwa mabingwa hao watetezi wakiondoka dimbani hapo na alama moja.
Uganda inapewa nafasi kubwa ya kushinda michuano hiyo ingawa sare ya leo imetoa mwanga kuwa michuano hiyo ni migumu na huenda ikitoa bingwa mpya msimu huu.
Michuano imeonekana kuwa migumu kuliko ilivyotarajiwa kwani katika michezo mitatu iliyochezwa mpaka sasa ni mabao mawili pekee yaliyofungwa.
Wenyeji Kenya walishinda mabao 2-0 jana dhidi ya Rwanda wakati timu ya Tanzania bara 'Kilimanjaro Heroes' itoka sare ya bila kufungana na Libya.
Zanzibar Heroes itacheza mechi yake ya kwanza kesho dhidi ya Rwanda wakati Kenya ikicheza na Libya katika michezo ya kundi A.
UGANDA NAO WAANZA KWA SARE CECAFA, WABANWA NA BURUNDI
Title: UGANDA NAO WAANZA KWA SARE CECAFA, WABANWA NA BURUNDI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) imeanza kwa sare michuano ya Cecafa Senior Challenge baada ya kubanwa mbavu na Burundi (Intamba Murug...
Post a Comment