SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SALAH JINO KWA JINO NA HAZARD, DE BRUYNE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah atapambana na nyota Eden Hazard, Kevin De Bruyne, Richarlison, Ashley Young na Xherden Shaq...
Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah atapambana na nyota Eden Hazard, Kevin De Bruyne, Richarlison, Ashley Young na Xherden Shaqiri kuwania tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Uingereza kwa mwezi Novemba.

Salah amefunga mabao saba mwezi huo katika michuano yote likiwemo goli dhidi ya timu yake ya zamani Chelsea katika uwanja wa Anfield.

Winga huyo raia wa Misri amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha tarakimu mbili kwa kufunga mabao baada ya kucheka na nyavu mara 16 katika mashindano yote.

Kura za kumpata mshindi wa tuzo hizo zimeanza kupigwa Ijumaa ya Disemba mosi na mwisho itakuwa usiku wa leo Novemba 4.

Salah anaweza kuwa mchezaji wa pili wa Liverpool kutwaa tuzo hiyo msimu huu baada ya Sadio Mane kufanya hivyo mwezi Agosti.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Bila shaka baada ya kuchukua ya mchezaji kwa chama cha wachezaji Wa kulipwa inayofata ni hii,ynwa

    ReplyDelete

 
Top