Michuano ya CECAFA Chalenji inaingia siku ya pili leo kwa mabingwa watetezi Uganda 'The Cranes' kucheza na timu ya Burundi katika mchezo wa kwanza wa kundi B.
Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika mwaka 2015 nchini Ethiopia na Uganda kuibuka na ushindi wa bao dhidi ya Rwanda 'Amavubi'.
Uganda wanaongoza kwa ubora wa viwango vya FIFA miongoni mwa timu zote za ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ambapo pia wanapewa nafasi kubwa ya kutetea taji hilo.
Mchezo huo utakuwa ni wa pekee kwa siku ya leo wa Michuano hiyo kabla ya kesho kupigwa mechi mbili.
Zanzibar Heroes watatupa karata yao ya kwanza kesho dhidi ya Rwanda katika mchezo wa kundi A na mechi nyingine ya kundi hilo hilo itakuwa kati ya wenyeji Kenya dhidi ya Libya.
MABINGWA UGANDA MZIGONI LEO CECAFA CHALENJI
Title: MABINGWA UGANDA MZIGONI LEO CECAFA CHALENJI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Michuano ya CECAFA Chalenji inaingia siku ya pili leo kwa mabingwa watetezi Uganda 'The Cranes' kucheza na timu ya Burundi katika ...
Post a Comment