Chama cha soka nchini Uingereza (FA) kimemtangaza mwamuzi Michael Oliver kuchezesha mchezo wa 'Manchester derby' kati ya Man United dhidi ya Man City utakaofanyika katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumapili.
Mtanange huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na uhasimu uliopo baina ya timu hizo huku zikitofautiana kwa alama nane kwenye msimamo.
Oliver 32, atasaidiwa na Beswick, Simon Bennett wakati mwamuzi wa akiba akiwa Jon Moss.
Mwezi Machi mwaka jana Oliver alikataa penati ya United mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya Marcus Rashford kuangushwa na mlinzi Martin Demichelis katika eneo la 18.
Novemba mwaka 2014, Oliver alimtoa kwa kadi nyekundu Chris Smalling na kumuacha mlinda mlango Joe Hart ambaye alienda kumpiga kichwa mwamuzi huyo.
City ndio vinara wa ligi hiyo ikiwa na pointi 43 ikifuatiwa na United yenye alama 35.
United itamkosa kiungo wake Paul Pogba baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Arsenal walioibuka na ushindi wa mabao 3-1 siku ya Jumamosi.
MICHAEL OLIVER KUZIHUKUMU UNITED, CITY JUMAPILI
Title: MICHAEL OLIVER KUZIHUKUMU UNITED, CITY JUMAPILI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Chama cha soka nchini Uingereza (FA) kimemtangaza mwamuzi Michael Oliver kuchezesha mchezo wa 'Manchester derby' kati ya Man Unite...
Post a Comment