Daktari wa timu ya Yanga, Edward Bavu amesema mlinzi Kelvin Yondani ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili au tatu zaidi kutoka sasa.
Yondani alipata maumivu ya kifundo cha mguu (enka) Disemba 7 katika mchezo dhidi ya Zanzibar Heroes wakati akiitumikia timu ya Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya Chalenji inayofanyika nchini Kenya.
Dk. Bavu ameiambia SDF Sports kuwa jana alikutana na mlinzi huyo na kumfanyia vipimo ambapo alibaini kuwa inabidi apate muda ili aweze kupona kabisa na kurejea dimbani.
"Yondani ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili mpaka tatu kutokana na kuuguza maumivu ya enka. Nadhani baada ya muda huo atakuwa fiti kabisa," alisema Dk. Bavu.
Hii ina maana kuwa mlinzi huyo atakosa mchezo wa hatua ya 64 bora dhidi ya Reha FC, Disemba 24 na pia anatarajia kukosa mechi ya ligi dhidi ya Mbao FC itakayopigwa katika uwanja wa CCM Kirumba.
Mbali na Yondani mchezaji mwingine aliye majeruhi kwenye kikosi cha mabingwa hao watetezi ni kiungo Thaban Kamusoko.
TAARIFA YA DAKTARI KUHUSU HALI YA YONDANI
Title: TAARIFA YA DAKTARI KUHUSU HALI YA YONDANI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Daktari wa timu ya Yanga, Edward Bavu amesema mlinzi Kelvin Yondani ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili au tatu zaidi kutoka sasa...
Post a Comment