Kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes', Moses Basena amesema wapinzani wao
Zanzibar Heroes ni timu imara uwanjani kuliko watu wanavyo fikiria.
Timu hizo zitakutana kesho kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Chalenji itakayopigwa katika uwanja Moi.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Simba amewaonya wachezaji wake kuwa Zanzibar ni ndogo kwenye karatasi lakini uwanjani ni tishio kwahiyo waingie uwanjani wakijua wanapaswa kupambana.
"Zanzibar wanacheza sana kitimu, aina yao ya mpira ni ngumu kuwazuia kwahiyo tunapaswa kuwa makini muda wote wa mchezo.
"Wanaonekana kama timu ndogo kwakua Uganda iko juu katika viwango vya ubora ukanda huu lakini uwanjani ni tishio na tumejipanga kwa lolote.
"Tunapaswa kushinda mchezo huu ni muhimu kwetu, tutacheza soka la kuvutia na kudhibiti mbinu zao zote ili tushinde," alisema Basena.
Uganda imeshinda michezo 12 kati ya 15 dhidi ya nchi zinazo zungumza Kiswahili katika michuano hiyo.
KOCHA WA UGANDA AIHOFIA ZANZIBAR NUSU FAINALI CHALENJI
Title: KOCHA WA UGANDA AIHOFIA ZANZIBAR NUSU FAINALI CHALENJI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes', Moses Basena amesema wapinzani wao Zanzibar Heroes ni timu imara uwanja...
Post a Comment