Miamba ya soka nchini timu za Simba na Yanga zimepangiwa timu kutoka Djibouti na Shelisheli katika hatua za awali ya michuano ya klabu bingwa Afrika na kombe la Shirikisho.
Yanga ambao ni mabingwa wa nchi watacheza na St Louis ya Ushelisheli katika klabu bingwa Afrika ikianzia nyumbani wakati Simba itacheza na Gendarmerie Nationale FC ya Djibouti.
Simba ambayo haijashiriki michuano hiyo kwa muda mrefu imepangwa na timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002 ambapo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Simba itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka mabingwa wa kombe la FA msimu uliopita.
Mabingwa wa Zanzibar timu ya JKU imepangiwa Zesco United ya Zambia ambayo nayo itaanzia nyumbani.
Kwa upande wa Zimamoto ambayo itashiriki michuano ya Shirikisho Afrika kutokea Zanzibar imepangiwa timu ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia.
SIMBA YAPELEKWA DJIBOUTI, YANGA SHELISHELI AFRIKA
Title: SIMBA YAPELEKWA DJIBOUTI, YANGA SHELISHELI AFRIKA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Miamba ya soka nchini timu za Simba na Yanga zimepangiwa timu kutoka Djibouti na Shelisheli katika hatua za awali ya michuano ya klabu bin...
Post a Comment