SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MOURINHO AKASIRIKA BAADA YA KUULIZWA KUHUSU MAN CITY
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho aliondoka kwa hasira kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kuulizwa kwanini aliingia ka...
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho aliondoka kwa hasira kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kuulizwa kwanini aliingia katika vyumba vya Man City baada ya kumalizika kwa derby ya Manchester wikiendi iliyopita.

Wachezaji wa City walikuwa wakishangilia ushindi wa mabao 2-1 kwa sauti ya juu pamoja na muziki hali iliyomfanya Mourinho kuwaingilia na kuwaambia waache kupiga kelele.

Mourinho hakufurahia kitendo hicho huku akisema hata wao walishinda mabao 3-1 dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates lakini hawakuonyesha utovu wa nidhamu.

"Kwangu mimi hilo swali ni la utashi wa magazeti, ni tabia ya mtu na sio zaidi ya hapo.

"Tulifanya nini kwenye uwanja wa Emirates ile tabia, kilitokea nini baada ya mechi? Tulikuwa na tabia za washindi lakini uliona wenzetu walichofanya," alisema kocha huyo mwenye maneno mengi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top