SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SAFARI YA UFALME WA NEYMAR ITAANZIA HAPA...
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Jana mashabiki wa soka Duniani walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa kuona droo ya hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa Ulaya yen...
Jana mashabiki wa soka Duniani walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa kuona droo ya hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa Ulaya yenye utajiri mkubwa  ikifanyika, nia yao ilikuwa kujua timu zipi zitapambana katika hatua hiyo ngumu.

Baada ya ratiba hiyo kutoka mechi hizo zilikuwa kama ifuatavyo,
Liverpool vs Porto, Chelsea vs Barcelona, Sevilla vs Manchester united, FC Basel vs Manchester City, Juventus vs Tottenham Hotspur, PSG vs Real Madrid, AS Roma vs Shakhtar Donetsk, Besiktas vs Bayern Munich.

Mchezo unataziwa kuwa mkubwa katika hiyo utakuwa kati ya mabingwa mtetezi Real Madrid dhidi ya matajiri wa Ufaransa PSG ambayo inaongozwa na nyota wa Kibrazil Neymar Jnr. Inawezekana watu wakaitazama kama mechi kali kwa maana ya ubora wa timu zenyewe lakini kwangu naiona kama safari ya Neymar kuutafuta ufalme wa soka Duniani.

Hakuna shaka uhamisho wa Neymar kwenda PSG ulichagizwa na mambo mawili, mosi ni pesa ambayo PSG imeilipa Barca na iliompa nyota huyo, sidhani kama kuna mwanasoka wa sasa angeweza kukataa kiwango cha pesa kilichowekwa mezani,lakini la pili ni uwepo wa Lionel Messi.

Pasi na shaka staa huyo aliona kuendelea kucheza pembeni ya Messi kusingemfanya kujitambulisha kama mwanasoka mahiri duniani kwakua raia huyo wa Argentina ndio kila kitu Barcelona, hili lilimfanya Neymar aamue kwenda kutafuta ufalme kwingine na mahala alipoona sahihi ni jiji la Paris.
Dunia ya sasa ya soka ina wafalme wawili(Messi na Cristiano Ronaldo) ili kuuvunja huu ufalme unapaswa ujitengenezee ufalme wako mwenyewe ingawa sio kazi rahisi kwakua inabidi kupambana ili kufikia mafanikio hayo.

Neymar anapaswa kuibeba PSG mgongoni kwake kuhakikisha anaivusha hatua hiyo mbele ya Real kama alivyosaidia Barcelona mwaka jana kupindua matokeo ya mabao 4-0 na kushinda 6-1 mbele ya mabosi wake wa sasa.

Njia ya kuuvunja ufalme wa Messi na Ronaldo uliodumu kwa takribani miaka kumi utaanza katika mechi hii, kasi ya Madrid inaonekana imepungua msimu huu hivyo kwa ubora wa kikosi cha PSG kwa sasa ambacho pia kina nyota wengine kama Kylian Mbappe na Edson Cavani ambao wametengeneza safu hatari ya ushambuliaji iliyopewa jina la 'MCN' lakini dunia itakuwa inamtazama zaidi Neymar kuliko wenzake.

Alimkimbia Messi ili ajenge ufalme wake sasa ni muda sahihi wa kuionyesha dunia kuwa maamuzi yake yalikuwa sahihi na pengine inawezekana Ballon D or ya mwakani tukapata mfalme mpya wa soka.

Haiwezi kuwa rahisi ila hana budi kuifanya, Ronaldo kafanya akiwa Madrid, Messi kafanya na Barcelona ni muda wa Neymar kuithibitishia dunia kuwa inawezekana akiwa PSG.

Tukutane mwezi Februari mwakani wakati mechi hiyo itakapopigwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top