SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MAVUGO KUIONGOZA BURUNDI MBELE YA KENYA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kwa mara nyingine kocha mkuu wa timu ya Burundi 'Intamba Murugamba' Oliver Niyungeko amemwanzisha mshambuliaji Laudit Mavugo katik...
Kwa mara nyingine kocha mkuu wa timu ya Burundi 'Intamba Murugamba' Oliver Niyungeko amemwanzisha mshambuliaji Laudit Mavugo katika kikosi chake kitakachocheza na wenyeji Kenya muda mfupi ujao kwenye uwanja wa Moi mjini Kisumu.

Timu hizo zinakutana kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Chalenji iliyoanza Disemba 3 nchini Kenya.

Mavugo ambaye anachezea klabu ya Simba ya Dar es Salaam ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha kocha Niyungeko ingawa amekosa nafasi ya kudumu msimu huu kwa Wekundu wa Msimbazi.

Mavugo, Fiston Razak na Hussein Shaban ndio watakao ongoza safu ya ushambuliaji ya Burundi katika mchezo huo ambao mshindi atatinga moja kwa moja fainali.

Kikosi kamili cha Burundi: Jonathan Nahimana (GK), Pierre Kwizera (C), Rachid Hererimana, Tresor Ndikumana, David Nsimirimana, Omar Moussa, Gael Duhayindavyi, Shasir Nahimana, Hussein, Mavugo na Fiston.

Wachezaji wa akiba: MacArthur Arakaza, Onesme Rukundo, Steve Nahimana, Youssuf Ndayishimiye, Bienvenue Shaka, Moussa Mossi, Moussa Haphizi Herimana, Cedrick Urasenga, Eric Ndoriyobija

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top