SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: PSG YAONJA KIPIGO ULAYA, BARCA, UNITED, JUVE SAAFI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
 Paris Saint Germain imekubali kipigo cha kwanza katika michuano ya klabu bingwa Ulaya kufuatia kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Bayern Mun...
 Paris Saint Germain imekubali kipigo cha kwanza katika michuano ya klabu bingwa Ulaya kufuatia kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Bayern Munich mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Allianz Arena.

Bayern ilipata bao yao kupitia kwa Robert Lewandowski na Correntin Tolisso aliyefunga mawili wakati Kylian Mbappe akifunga bao la kufutia machozi la PSG.

Pamoja na kipigo hicho PSG imeendelea kubaki kileleni mwa kundi C na alama 15 sawa na Bayern lakini wakiwa na uwiano wa mabao ya kufunga.

Barcelona ikiwa Nou Camp imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sporting CP wakati Juventus ikipata matokeo kama hayo mbele ya Olympiacos.
Manchester United ikiwa Old Trafford imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya CSKA Moscow huku Chelsea ikibanwa na Atletico Madrid kwa kulazimishwa sare ya bao moja kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Matokeo ya mechi zote za UCL

Benfica 0-2 Basel
Man United 2-1 CSKA Moscow
Bayern Munich 3-1 PSG
Celtic 0-1 Anderlecht
Chelsea 1-1 Atletico Madrid
Roma 1-0 Qarabag FK
Barcelona 2-0 Sporting CP
Olympiacos 0-2 Juventus

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top