SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MUDATHIR ATOBOA SIRI YA KIWANGO CHAKE..
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo aliye kwenye kiwango bora Mudathir Yahya amesema siri yake kubwa iliyomfanya kufika hapo ni kuaminiwa na kocha wake Hans van Pluijm...
Kiungo aliye kwenye kiwango bora Mudathir Yahya amesema siri yake kubwa iliyomfanya kufika hapo ni kuaminiwa na kocha wake Hans van Pluijm wa Singida United.

Mudathir ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya na kikosi cha Zanzibar Heroes kwenye michuano ya Chalenji amegeuka kuwa nyota muhimu kuanzia kwenye klabu hadi timu za taifa.

Kiungo huyo amesema kuwa hakuna kitu kilicho ongezeka kwake zaidi ya kuaminiwa na kocha hivyo kwa nafasi kubwa anayopata ndio inayomfanya kufanya vizuri.

"Mtu unavyo aminiwa unajiona kama una deni kubwa kwa kocha kwahiyo unapambana ili usimuangushe, unapopata nafasi ndio unaonyesha uwezo wako kama hivi," alisema Mudathir.

Mudathir alifunga bao la kwanza katika ushindi wa jana wa mabao 3-1 uliopata Zanzibar Heroes dhidi ya Burundi huku akionyesha kiwango safi kwenye mchezo huo wa kundi A.

Licha ya Singida United kufanya usajili mkubwa msimu huu lakini Mudathir amegeuka kuwa chaguo la kwanza la kocha Hans mpaka kuamua kumpa kitambaa cha unahodha.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top