SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: AZAM YAIPA KONGOLE SIMBA KWENYE HILI....
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa Klabu ya Azam imeipongeza Simba kwa kubadili mfumo kutoka umiliki wa wanachama hadi uwekezaji ambapo mfanyabiashara Mohammed De...
Uongozi wa Klabu ya Azam imeipongeza Simba kwa kubadili mfumo kutoka umiliki wa wanachama hadi uwekezaji ambapo mfanyabiashara Mohammed Dewji alishinda zabuni.

Simba imekuwa klabu ya kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kuingia katika mfumo huo ambao unatumiwa na timu nyingi zilioendelea kote duniani hali ambayo inategemewa kuwaona Wekundu hao wakifanya vizuri kwenye michuano ndani na nje ya nchi kuanzia mwakani kutokana na uwekezaji utakaofanyika.

Msemaji wa klabu hiyo, Jeffer Idd amesema kuwa Simba imepiga hatua kubwa ambayo matunda yake wataanza kuyaona muda si mrefu kutoka sasa.
"Kwa niaba ya uongozi wa klabu ya Azam nichukue nafasi hii kuipongeza Simba kwa hatua kubwa waliopiga kwa kuingia katika mfumo wa hisa ambao utakuwa wa kibiashara na faida yake itaonekana muda mfupi tu.

"Ni jambo jema kumpongeza mwenzako anapofanya vizuri, nina amini Simba wameonyesha njia na wengine watafuata," alisema Jaffer.

Klabu za Singida United na African Lyon nazo ziliipongeza Simba kwa hatua hiyo muda mfupi baada ya kufanya maamuzi hayo siku ya Jumapili.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Hahaaaaa....team zoote zitatuma pongezi ila kuna team haiwezi fanya hivyo kwakua imewauma sana heheeee

    ReplyDelete

 
Top